Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kaingia katika historia ya Dar es Salaam katika kifo chake. Bahari ya watu walijazana Msikiti wa Kichangani kuja kuswalia jeneza lake na kisha kulifata nyuma jeneza hilo hadi Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa. Sheikh Ilunga ni mgeni katika mji wa Dar es Salaam kwa maana ya kuwa hakuzaliwa Dar es Salaam wala hakuwahi kuishi Dar es Salaam. Alikuwa akija na kuondoka zamani akirejea kwao Tabora na baadaye kuhamia Mwanza, akija Dar es Salaam na kurejea Mwanza.